Kiswahili

Covid-19: Ujumbe kwa Ulimwengu

Wapendwa mabibi na mabwana katika ubinadamu,

Barua hii imetumwa kutoka kwa wanazuoni wa Kiislam, walimu, wahadhiri na wafikiriaji kutoka sehemu mbalimbali duniani. Tunawaombea muwe na afya njema na muwe salama kutokana na virusi vya korona (ugonjwa ambao kitaalamu unaitwa COVID-19). Tunathamini usalama wenu, furaha na ustawi wenu; kutokana na roho hii ya kujali ndiyo tukaandika barua hii.

Tupo katikati ya janga la kidunia. Virusi vya korona  vipo karibu katika kila nchi ya dunia. Watu wanaweza kufa pindi wakiambukizwa na ugonjwa huu kuliko kama wangembukizwa na mafua. Hofu na wasiwasi vimetawala maisha yetu ya kila siku. Nchi zimeweka vizuizi, shule zimefungwa na maisha ya kijamii yamevurugika. Wengi watapoteza wapendwa wao. Wengi watafariki kabla ya kuaga.

Wengi wetu wameonesha huruma na umoja, bila ya kujali tofauti zetu. Hii ni sababu ya sisi kuamini kuwa, hata katika vipindi hivi visivyo vya kawaida, virusi vya korona vinaweza kuwa njia ya muamko wa kiakili na kiroho. Kinachofuata ni nukta muhimu sisi kuzingatia. 

Tunamtegemea Mwenyezi Mungu

Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa.

Qur’an, Sura ya 35, Aya ya 15

Virusi vya korona vimetufanya tutambue kuwa sisi hatujitoshelezi. Kuna vitu hatuviwezi na ni wahitaji. Uwepo wetu na uwezo wetu wa kufanya kazi unategemea karibu idadi ya vitu vingi visivyo na kikomo; vitu ambavyo hatuwezi kuvidhibiti na hatuna nguvu navyo. Vitu vyote hivi hatimaye vinamtegemea Mwenyezi Mungu. Kwakuwa Mwenyezi Mungu ametuumba sisi na vitu vyote tulivyovitaja hapo juu, kuishi kwetu kunamtegemea Yeye tu.Sisi hatujitoshelezi, hata kama baadhi yetu wakipotoshwa kwa kufikiri kuwa tunaweza.

Kwani hakika mtu huwa jeuri, Akijiona katajirika.”Qur’an, Sura ya 96, Aya ya 6 na 7

Dunia yote imegeuka chini juu kufuatia punje moja ya RNA. Virusi hivi vidogo, ambavyo hatuwezi kuviona kwa macho, vimeathiri karibu kila nchi duniani. Hakuna kinga kwa sasa. Uchumi unaelekea kuporomoka na mifumo ya afya imezidiwa. Watu wanauoga na wasiwasi. Watu wengi wametakiwa kubaki nyumbani. Hakuna kiwango cha pesa na nguvu katika dunia hii kinaweza kubadilisha kinachotokea. Hii itufundishe somo muhimu, hususani kwa wale walio na kiburi: lazima tuwe wanyenyekevu. Kikwazo kikubwa cha muongozo wa kiroho na rehema ni udanganyifu wa kujitosheleza mwenyewe, ambao kwa kiasi kikubwa umetawaliwa na kujikweza na kiburi.

Na kwa yakini tulipeleka [Mitume] kwa kaumu zilizokuwa kabla yako, kisha tukazitia katika dhiki na mashaka ili zipate kunyenyekea [Kwetu].

Qur’an, Sura ya 6, Aya ya 42

Virusi vya korona na alama za Mwenyezi Mungu

Wengi wetu hatujawahi kuviona virusi moja kwa moja. Hatakama vinaonekana kwa darubini ya kielekroniki, wengi wetu tunategemea vitabu vya kisanyansi na picha, na yale tunayoambiwa na wataalamu. Hatahivyo, tunaona na kuhisi athari za virusi. Hii inatosha kwa yeyote kuhitimisha kuwa virusi vipo. Pia tunachukua hatua kujikinga na kuwakinga wengine kuambukizwa na ugonjwa huu usioonekana. Tukiitumia hii kwa Mwenyezi Mungu, sio tu kwamba tuna ufahamu wa ndani wa uwepo Wake, tunaweza kuona na kuhisi athari za ukweli Wake.

Tunaishi katika ulimwengu huu mzuri. Tuna matumaini, upendo, tunatafuta haki na kuamini katika thamani ya juu ya maisha ya mwanadamu. Tunafikiria, tunapata ukweli, tunapata hitimisho na kugundua. Tunaishi katika ulimwengu mkubwa wenye mabilioni ya sayari, nyota na galaksi. Ulimwengu una sheria na misingi imara ambayo, hatakama ingekuwa tofauti kidogo, ingeweza kuokoa dharura za kiufahamu, kuyajua maisha. Tunaishi katika sayari yenye lugha zaidi ya 6,000 na zaidi ya viumbe milioni nane. Tunahisi – kutoka ndani kabisa – ubaya wa kufanya makosa, na uzuri wakufanya mambo mazuri.

Hizi zote ni alama za uwepo wa Mwenyezi Mungu na ukubwa wake.

Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanaozingatia.

Qur’an, Sura ya 2, Aya ya 164

Maisha, kifo na kusudi

Virusi vya korona vimekuwa chanzo na inawajibika kwa vifo vingi. Tumeona idadi ya vifo ulimwenguni ikiongezeka kwa kiwango cha kutisha siku baada ya siku. Hii imezua hofu na wasiwasi. Lakini imetengeneza fursa kwetu kutafakari asili ya uwepo wetu, na kutafakari kifo na uhai.

Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Kiyama. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu.

Qur’an, Sura ya 3, Aya ya 185

Kuukataa ukweli kwamba maisha yetu ya kusudi maalumu ni kitu cha ajabu na kwenda kinyume na uhalisia. Sisi ni viumbe tunaoendeshwa na makusudio. Tunafanya kila kitu kwa malengo, kutoka kusafisha meno yetu mpaka kununua gari, lakini bado kuna watu ambao hawa amini kuwa kuna kusudi la uwepo wetu. Bila kuwa na kusudi maalumu basi hakuna sababu ya uwepo wetu, na tunapoteza maana halisi ya maisha yetu. Kukataa kusudi kuu kwa misingi ya uwepo wetu wakati tukiamini katika makusudio yaliyo tengezwa na watu katika maisha yetu, kwa tafsiri ni, kujipotosha mwenyewe. Haina tofauti na kusema, “Tujifanye kuwa tuna makusudio.”

Mola Wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure.

Qur’an, Sura ya 3, Aya ya 191

Kwa hiyo Kusudi letu nini ni?

Virusi vya korona vimetufanya tuifikirie, na kuvihifadhi, vitu tunavyovihitaji, upendo na heshima. Vingi kati ya hivi ni vitu tunavyoviabudu. Hata watu wasioamini Mungu, wanadhihirisha dalili za kuabudu, kuheshimu na kujitoa kwa vitu. Kitu tunachokipenda na kukiheshimu sana, pamoja na chochote tunachokipa nguvu ya juu kabisa na kuamini kuwa ndio tunachokitegemea kwa kiasi kikubwa, hicho ni kitu tunachokiabudu. Kwa watu wengi, hii inaweza kuwa itikadi, kiongozi, mwanafamilia, au wao wenyewe. Ushirikina na kuabudu sanamu sio tu kuyaabudia au kusujudu mbele ya kituchenyewe.

Na katika watu wapo wanaochukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana.

Qur’an, Sura ya 2, Aya ya 165

Kimsingi Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba tusipomuabudu Yeye, tutaishia kuabudu kitu kingine. Hivi vitu vinatufanya ‘watumwa’ na vikawa ‘mabwana’ zetu.

Je! Umemuona aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake?

Qur’an, Sura ya 45, Aya ya 23

Hata wale wanaojiita wasioamini Mwenyezi Mungu wanamuabudu mtu au kitufulani, pengine kwa kutojua. Kitu hicho huenda kikawa ni matamanio yao wenyewe. Tunapokataa ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kukataa kubadilika, iwe kwa kiburi au mapenzi ya ulimwengu huu wa vitu, tumeyafanya matamanio yetu yatutawale. Tumekuwa watumwa wa matamanio yetu.

Mwenyezi Mungu, ambaye anajua kila kitu, tukiwemo sisi, na ambaye  ni Mwingi wa Rehema, anatuambia kuwa yeye ndiye mmiliki, na kuwa kwa kumuabudu Yeye tu ndiyo tutajiweka huru kutokana na minyororo ya vitu tulivyovifanya kuwa ni mbadala Wake.

Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.

Qur’an, Sura ya 51, Aya ya 56

Kumuabudu Mwenyezi Mungu ndiyo kusudio la maisha yetu. Mwenyezi Mungu amejikita ndani kabisa ya asili yetu, na pale Mwenyezi Mungu anapotuamrisha kumuabudu Yeye basi hiyo ni huruma na kitendo cha upendo. Pindi tukiijaza mioyo yetu kwa hofu na mapenzi ya Mwenyezi Mungu tutajihisi na amani na tutapata utulivu ambao hauelezeki, na amani ambayo haitikiswi na majanga.

Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Ati yupo muumba mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayekupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu ila Yeye tu. Basi wapi mnakogeuzwa? 

Qur’an, Sura ya 35,Aya ya 3

Acheni ufisadi na udhalimu

Janga hili halijatokea kwa bahati mbaya. Matendo yetu binafsi na ya ujumla ndio yanayosababisha yanatokea kwenye dunia yetu. Hili linatakiwa litufanye tufikirie juu ya tuliyoyafanya, na ambayo hatujayafanya, ambayo yanaweza kuwa chanzo cha janga hili. Kwa kuwa tunamtegemea Mwenyezi Mungu na uhusiano wetu na vitu vingine, yakiwemo mazingira yetu pamoja na watu wengine, lazima tugundue kwamba ni ufisadi na udhalimu wetu ambao unaweza kuwa umechangia katika janga hili.

Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyoyafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyoyatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.

Qur’an,Sura ya 30, Aya ya 41

Dunia yetu ipo katika hatihati ya kuteketea. Kiwango cha uchafuzi wa mazingira unaharibu na kuhatarisha majumba yetu. Udhalimu na vita vimetanda. Mamilioni ya binadamu wenzetu wamekuwa wakimbizi, mamilioni wameuwawa katika mitafaruku na mamilioni hawana chakula cha kuwatosheleza kuishi. Wote kwa ujumla tunahusika kwa kuweka jitihada za kutosha katika kuzuia uovu, na wengi wetu tunahusika moja kwa moja katika kuusababisha uovu huo. Lazima tuwajibike na tuelewe kwamba janga hili ni ishara, ishara ya Mwenyezi Mungu kutuonya tuache udhalimu na ufisadi katika ardhi.

Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa.

Qur’an,Sura ya 7, Aya ya 56

Lazima tutambue kwamba sisi ndio tunahusika na kuitunza ardhi. Ina maanisha kwamba ni jukumu letu kuleta usawa, mpangilio na kutokuwa wabadhirifu. Vita vya kidhalimu lazima viishe, mauaji ya watu wasio na hatia yaachwe, sera za uchumi zenye uonevu zifutwe, uonevu wa wanyama usitishwe, ubadhirifu na tamaa vimalizwe. Tunakumbana na maamuzi ya kufanya. Aidha kuufuata muongozo wa Mwenyezi Mungu, ambao utairudisha hali ya usawa au kuendelea na ufisadi.

Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.

Qur’an,Sura ya 13, Aya ya 11

Muamini Aliye Muaminifu

Janga hili la dunia limetugandisha kwenye skrini zetu tukisubiri sasisho mpya na muongozo wa wataalamu; watalamu wa virusi, wataalamu wa magonjwa ya milipuko na watu wengine wenye mamlaka. Tunayaamini watakayoyasema na tunafuata maelekezo yao. Lakini, wengi wetu hatuna uwezo wa kuthibitisha ukweli wa kauli zao. Hatuna msingi wa kitaaluma wala utaalamu wa kuweza kufanya hivyo. Hatuwezi kujua kila kitu kutokana na mapungufu yetu ya kibinaadamu. Kutegemea ushuhuda wa watu ni kitu kisichoepukika na muhimu kwa ajili ya uwepo wetu. Kwakuwa tunaweza kuamini ushuhuda wa mtu, basi inaleta mantiki zaidi  kumuamini ambaye ni muaminifu zaidi ya watu tunaowaamini kwa sasa.

Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Qur’an, Sura ya 48, Aya ya 29

Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alipewa utume zaidi ya miaka 1400 iliyopita, akiwa na ujumbe mrahisi lakini mkubwa usemao hapana Mola anayestahili kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Mtume Muhammad  (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ni mjumbe wake wa mwisho. Tunashauri msome kwa kina historia ya Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) iliyoandikwa kwa mapana, ambayo itatudhihirishia taarifa ya kutosha kuhusu ukamilifu ya tabia yake. Hakuwa muongo wala mtu aliyepotoshwa, lakini alikuwa wa mwisho miongoni mwa mitume na manabii kama Nuhu, Ibrahimu, Musa na Issa (Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote). Walihubiri upweke (umoja) wa Mwenyezi Mungu. Mshikamano wa binadamu unadhirika zaidi pale ambapo wanauyakinisha ukweli.

Kuyasoma maisha ya Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na muongozo wake kutakudhihirishia kwamba alitumwa na Mwenyezi Mungu na hivyo kuwa ushahidi wa kutosha kwamba Qur’an ni kitabu cha mwisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa kuzingatia hoja za hapo juu, kuukana ujumbe wa Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) , kimantiki utakuwa sawa na kukataa taarifa ambazo tumekuwa tukizisikiliza kwa makini kutoka kwa wataalamu, katika janga hili.

Virusi vya korona vinaweza kukupeleka peponi

Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenyenguvu na Mwenyemsamaha.

Qur’an,Sura ya 67, Aya ya 2

Mwenyezi Mungu ametuumba tumuabudu, na sehemu ya kumuabudu ni kupewa mitihani na majaribu kama janga hili la dunia. Kufaulu mtihani huu, kwa kukabiliana nao katika njia inayomridhisha Mwenyezi Mungu, kunaweza kutuwezesha kuyapata makazi yetu ya kudumu peponi. Dunia ni uwanja wa mitihani wa majaribu ambayo yapo kama njia ya kukuza wema, kuhakikisha makuzi ya kitabia na kiimani na kuamua nani miongoni mwetu kweli anastahili furaha ya milele. Katika nyakati hizi ngumu, lazima tuwe wavumilivu na wenye ujasiri na tuonyeshe huruma kwa wale walioathirika na virusi hivi kwa kuwasaidia kwa njia yoyote kadri tuwezavyo.

Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyowajia wale walio pita kabla yenu? Ili wapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walioamini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipokaribu.

Qur’an,Sura ya 2,Aya ya 214

Uislamu unawezesha. Unaona mateso, uovu, madhara, maumivu na matatizo, kama mitihani na unayaona haya kama ishara ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema “Mwenyezi Mungu akimpenda mja (Wake) humpa mitihani.”

Mwenyezi Mungu humpa mitihani mja wake ampendae kwa kuwa mitihani hiyo ndio njia ya kuingia peponi; na kuingia peponi ni kutokana na mapenzi na huruma ya Mwenyezi Mungu. Ndio maana mtihani huu wa COVID-19 unaweza kutusaidia kuipata pepo. Lakini tusipoweza kuyakabili majaribu haya baada ya kujitahidi kadri tuwezavyo, huruma na haki ya Mwenyezi Mungu itatuwezesha kulipwa kwa kiasi chake, aidha katika maisha haya au ya baadae yanayotusubiri.

Muamko

Na tutawaonjesha adhabu khafifu kabla ya adhabu kubwa, huenda labda watarejea. Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anayekumbushwa kwa ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa?

Qur’an,Sura ya 32,Aya ya 21 na 22

Janga hili la dunia lazima lisababishe muamko wa kiimani na kiakili. Ni muda wa kurejea  katika njia ya Mwenyezi Mungu. Mtihani huu tuliopewa na Mwenyezi Mungu unaweza kuwa ishara ya mapenzi yake au ishara ya kiburi chetu. Kama tutakuwa wanyenyekevu, wavumilivu huku tukitarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kumuabudu kwa dhati, kuonyesha huruma na kufanya vitu sahihi, tutafaulu mtihani huu na hivyo kustahili kuupata utulivu wa milele peponi. Sehemu ambayo ina utulivu kiasi cha kwamba kama kuna ambaye aliteseka zaidi kuliko watu wote duniani, na akaingizwa humo kwa wasaa mfupi tu, basi atapiga kelele huku akisema “Sijawahi kuteseka”, kama tulivyoambiwa na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).

Maamuzi ni yetu. Tunaweza kuukubali ukweli kwamba Mwenyezi Mungu ndiye pekee anayestahili kuabudiwa kwa haki na kwamba Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake)  ni mtume wake wa mwisho, au tunaweza kuukataa ukweli na hivyo kuelekea motoni, kwa kuwa tumechagua kuukana muongozo wa Mwenyezi Mungu na rehema zake. Huu ndio muda wa kumuamini na kumkumbuka. 

Na anayemcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia.

Qur’an,Sura ya 65,Aya ya 2 na 3

Mwenyezi Mungu atuongoze na atulinde sote, na atujaalie miongoni mwa wanaostahili rehema yake maalumu.

Imesainiwa

Mufti Muhmmad Taqi Usmani, vice president of Darul Uloom University Karachi, Pakistan. The most Influential Muslim in 2020 according to www.themuslim500.com.

Sheikh Dr Sharif Ibrahim Saleh Alhussaini CON, Grand Mufti of Nigeria,  Chairman, Fatawa Committee of the Supreme Council for Islamic  Affairs of Nigeria, Chairman, Assembly of Muslims in Nigeria AMIN.

Muhmmad Seydya Suliman al-Nawawi al-Shanqiti, vice president of Association of Muslim scholars.

Hussain Yee, president of Serving Mankind Association, Malaysia.

Dr. Ali Muhammad Muhammad al-Sallabi, Muslim historian and religious scholar, Libya.

Dr Zakir Naik, Founder, Peace TV Network, Malaysia.

Dr Mohd Asri bin Zainul Abidin, Mufti of Perlis, Malaysia.

Abdul Raheem Green, international preacher, UK.

Sheikh Dr AbdulHayy Yusuf, Vice president of the board of the scholars of Sudan.

Dr Muhmmad Yusri Ibrahim, Academic and researcher, Egypt.

Daei al-Islam al-Shahhal, scholar, Lebanon.

Dr Haifaa Younis, Jannah institute, St. Louis, MO, USA.

Dr. Yasir Qadhi. Dean, The Islamic Seminary of America Dallas, TX, USA.

Sheikh Shadi Alsuleiman, Chairman of Australian National Imams Council (ANIC), Australia.

Dr Muhmmad Salah, Huda TV, Egypt.

Hamza Tzortzis, author and international preacher, UK.

Dr Tawfique Chowdhury, Australia.

Sheikh Omar Suleiman, Founder & President of Yaqeen Institute for Islamic Research, USA.

Imam Said Rageah, Chairman of Journey of Faith international conference, Chairman and founder of Sakinah Foundation, Toronto Canada.

Fadel Soliman, Director of Bridges Foundation, Egypt.

Dr. Anas Altikriti, CEO and founder, The Cordoba Foundation, United Kingdom.

Sheikh Zahir Mahmood, founder and teacher at As-Suffa Institute. Birmingham, England.

Sheikh Dr Haitham al-Haddad, founder of AlMarkaz for Revival and Reform Studies, UK. 

Sheikh Mohammed Abdullah Houiyat, scholar, Germany

Dr Kamil Salah, lecturer in Islamic jurisprudence University of Jarash, Jordan.

Sheikh Ihsan Mohammed Alotibie, scholar, Jordan.

Nour al-Din Yildiz a scholar and a preacher, Turkey.

Shaykh Asrar Rashid. Founder of Hadithiyya Institute, Imam at Jamatia Islamic Centre Birmingham. Author, theologian and orator, UK.

Muhammad Idrees Zubair, former professor and member BOG of IIU, Islamabad, Pakistan.

Dr. Bachir Aissam Almorrakochi, scholar, author and the director of Irshad Academy for studies and development, Morocco.

Shaykha Dr. Tamara Gray, Executive Director, scholar and chief spirituality officer of Rabata.

Imam Siraj Wahhaj, Masjid Al Taqwa New York.

Imam Dr. Khalil Abdur-Rashid, Muslim Chaplain at Harvard University, Instructor of Muslim Studies at Harvard Divinity School & Adjunct Professor of Public Policy at Harvard Kennedy School.

Follow us

Messenger icon
Send message via your Messenger App